Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551125

Habari za Mikoani of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gereza Katavi laelemewa wafungwa

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda, amesema Gereza la Mpanda mkoani Katavi, limeelemewa na wafungwa kwani uwezo wake ni kubeba wafungwa 100 tu lakini hadi sasa lina wafungwa 400.

Pinda ameeleza kuwa serikali imejipanga kujenga magereza mawili ili kupunguza changamoto hiyo ambayo kwasasa inaonekana dhahiri kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mapema mwanzo wa juma hili, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, alizungumza kuhusu uendeshwaji wa kikoloni katika magereza mengi nchini, ukiwemo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa kwa wafungwa wengi.

Lakini pia Hayati John Pombe Magufuli, aliwahi kutembelea Magereza na kususisitiza kuhusu wafungwa kutendewa haki, huku akisisitiza kuwepo kwa miundombinu bora magerezani.