Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540235

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: ippmedia.com

Gunia tano za bangi zakamatwa Longido

Akizungumza na Nipashe meneja ambaye ni askari wa hifadhi hiyo, Peter Millanga, amesema majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo, askari wamefanikiwa kukamata pikipiki ikiwa na gunia tano za bangi eneo la Engutukoit ukanda wa Ngereyan ambazo zilikuwa zikisafirishwa kwa njia za panya kuelekea Kenya.

"Mhusika hakuweza kukamatwa kwani alipozidiwa alitelekeza pikipiki na mzigo wake na kufanikiwa kukimbia," amesema Millanga.

Millanga amesema kwa mujibu wa askari walioshiriki kwenye doria hiyo, wamesema walipokea taarifa toka kwa msiri wao (informer) na kuamua kuifanyia kazi taarifa hiyo ndipo walipofanikiwa kukamata magunia.

Join our Newsletter