Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 05Article 555370

Siasa of Sunday, 5 September 2021

Chanzo: MillardAyo

Gwajima: Nimeonekana jitu baya

Mbunge wa kawe na Askofu  wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima Mbunge wa kawe na Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

Niliitwa na Kamati ya Maadili ya Bunge wiki iliyopita nilipotoka wengi mliniuliza kimejiri nini na nikasema sitosema hadi Kamati iseme kwanza na kwasababu Kamati imeshaongea acha nami nizungumze”

“Sababu ya kuongea ni kwasababu wameniongelea kama Mtu mbaya sana, Jitu baya sana ambalo kama lipo kama lilivyotajwa basi halitakiwi hata kuwa Kiongozi wa Kanisa”

“Mimi Mchungaji wa muda mrefu sana hapa tu Ubungo nipo kwa miaka 25, nilipoitwa kwenye Kamati yale niliyoitiwa ni kuhusu mahubiri ya Kanisani, Mimi nikawaambia sidhani kama Kamati mmefanya vizuri maana yote nimeongea Kanisani na hakuna mwenye Mamlaka ya kuuliza maswali juu ya Ibada ya Kanisani na imani za Watu na nikasema kwenye hili Kamati mmekosea”

“Niliwaambia Kamati mmesema mmesikia nimewaambia Watu wasichanjwe nikasema hiyo haibadiliki milele, nikaweka wazi kwamba sisi Ufufuo na Uzima chanjo ni hiari na sisi tumechagua hatuchanji sikupindisha nilisema hatutowaruhusu Waumini kuchanja na sababu zetu ni hatujapata taarifa za kutosha juu ya madhara ya chanjo ya muda mfupi, siku zijazo na siku nyingi”

“Kwahiyo kama nimeitwa mkorofi ukorofi wangu ni huo na kama huo ndio ukorofi basi ni ukorofi kwelikweli kwenye eneo hilo, wakaniambia jitetee nikasema sina la kujitetea, siwezi kujitetea kwa mahubiri niliyohubiri yanatoka kwa roho mtakatifu, nimefafanua ili mjue Gwajima sio mkorofi ".