Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553315

Siasa of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gwajima na Slaa wavuliwa ujumbe Kamati ya Maadili ya Bunge

Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe na Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe na Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga

Wabunge Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

Wabunge hao wameitwa mbele ya kamati hiyo wakituhumiwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge, jambo ambalo kwa mujibu wa kanuni za kamati hiyo, moja kwa moja wanakuwa wamepoteza sifa za kuwa wajumbe.

Gwajima alianza kuhojiwa jana na kamati hiyo kwa zaidi ya saa mbili na ataendelea kuhojiwa tena hii leo huku Slaa nae akitarajiwa kuhojiwa pia hii leo.