Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 20Article 543517

Habari Kuu of Sunday, 20 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Haiingii akilini Vyama vya Ushirika vinatengeneza Mabilioni ila haviwasaidii" Bashe

"Haiingii akilini Vyama vya Ushirika vinatengeneza Mabilioni ila haviwasaidii" Bashe

Waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao.

Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama.

“Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae pia alitaka vyama hivyo kuanzia mwakani vianze kuwanufaisha wakulima  badala ya kuendelea kuwekeza fedha kwenye miradi isiyo na tija” Bashe

“Mnajua haiingii akilini kabisa kuona kwamba vyama vya ushirika vinatengeneza mabilioni kupitia makato ya wakulima lakini vinashindwa kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hata zile muhimu za kifamilia. Fedha zote zinaenda kulipa madeni ambayo kimsingi yamezalishwa na viongozi wanaoongoza vyama hivi kwa maslahi yao binafsi…naomba hili lifike mwisho sasa.’’ Bashe

Akizungumzia changamoto ya matumizi mabaya ya mikopo kwenye vyama vya ushirika, Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kuendesha mafunzo kuhusu namna bora ya kutumia mikopo kabla ya kuwapatia walengwa hatua ambayo imesaidia sana kupunguza tatizo hilo.

“Pamoja na mambo mengine lengo la mikopo yetu huwa kuhakikisha tunamsaidia mlengwa kukuza mtaji wake na kufanya shughuli zake kwa ufanisi na ushindani ili atengeneze faida itakayomuwezesha kurejesha fedha kwetu bila changamoto. Hili kufanikisha hili wateja weteja wetu zikiwemo AMCOS wamekuwa wakipata mafunzo ya namna bora ya kuendesha shughuli zao kutoka kwa wataalam tunaoshirikiana nao…hii imesaidia sana!’’ alitaja.Benki hiyo mbali na kuwa moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo, ilipata fursa ya kuelezea huduma zake mbalimbali kwa wadau hao ikiwemo huduma ya NBC Shambani    inayolenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

“Lengo hasa la huduma hii ya NBC Shambani ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya  vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.

“Akaunti  ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada  ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa  faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima  wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.

Wakizungumzia huduma za kifedha, baadhi ya wadau wa kilimo walisema huduma hizo ni muhimu kwa kuwa kwasasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo biashara ambacho ustawi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinaenda sambamba na mahitaji wa wadau hao.

“Huduma kama NBC Shambani zinatugusa wadau wote tukiwemo  hata sisi wafanyabiashara wa mazao ya kilimo na usindikaji. Hii ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimo tunahitaji haswa!,’’ Shakiru Kyetema, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shayakye Trading Company inayojihusisha na uuzaji wa kahawa.

EXCLUSIVE: MZEE AJENGA NYUMBA JUU MTINI, ‘ULAYA NDOGO’, WATU 50 WANAKAA, INA TV, JIKO, MKE KAKIMBIA