Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 10Article 542035

xxxxxxxxxxx of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Haniu ateuliwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).

Kwa mujibu wa taarifa ya taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa, kabla ya uteuzi huo Haniu alikuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Kampuni ya Africa Media Group Limited.

Haniu anachukua nafasi ya Msigwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, uteuzi huo wa Haniu unaanza jana Juni 9, 2021.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Profesa Eleuther Mwageni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Profesa Mwageni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Profesa Esther Ishengoma aliyemaliza muda wake, na uteuzi wake ulianza Juni 7, mwaka huu.

Pia Rais Samia amemteua Dk Neema Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani. Dk Mwita amechukua nafasi ya Dk Theodora Mwenegoha aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Uteuzi wake umeanza Juni 8, 2021.

Join our Newsletter