Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584950

Siasa of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hatimaye! Zungu ajitosa Uspika- VIDEO

Hatimaye! Zungu ajitosa Uspika Hatimaye! Zungu ajitosa Uspika

Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar Es Salaam Mhe. Mussa Azzan Zungu leo Januari 11,2022 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Mhe. Job Ndugai baada ya kujiuzuru Januari 6,2022

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu hiyo Makao makuu ya chama cha Mapinduzi(CCM)Jijini Dodoma Mhe.Zungu amemshukuru mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika kwani kwa Mujibu wa katiba ya Taifa na kwa mujibu wa Chama cha Mapinduzi nafasi hiyo inautaratibu wake wa kuomba na hivyo ndivyo alivyofanya kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu zote zinazohitajika.