Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560338

Habari Kuu of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hii hapa kampeni ya kuhamasisha ulipaji mikopo kutoka HESLB

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu imeanzisha kampeni inayokwenda kwa jina la Sifurisha yenye lengo la kukusanya billion 185 za kuwasaidia wanafunzi walionufaika na mkopo mwaka 2021/22.

Kampeni hiyo iliyoanza Septemba 28, inalengo la kuwahamasisha wanaodaiwa mikopo waweze kukamamilisha mikopo hiyo huku ikizingatia sheria ya Serikali inavyowataka watu walionufaika na mikopo hiyo.

Mnamo mwezi July 2021 Wizara ya Elimu ilitoa baadhi ya makato katika mikopo ya elimu ya juu ikiwa ni utekelezaji wa tamko la Rais Samia aliloiagiza bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu.

Kitendo hicho kinamaanisha maelfu ya wanufaika ambao walihitajika kulipa mamilioni ya fedha ikiwa ni sehemu ya marejesho ya mkopo huo angalau wamepata faraja.Hata hivyo ni jambo lisiloepukika kuwa bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatakiwa kutafuta mbinu mbadala kuhakikisha wadaiwa wanarejesha kiwango cha mikopo walichokopeshwa ili kuiwezesha taasisi hiyo kuwafikia walengwa wengi zaidi kila mwaka.

"Kampeni hii inawalenga wadaiwa wote ikiwa na lengo walipe madeni yao baada ya malipo ya ziada levy tax kuondolewa, kwahiyo tunakuja na njia rahisi ya kuwahamasisha kulipa na wengine kumaliza kabisa" , amesema Afisa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo Veneranda Malima.

Amesema wana mpango wa kuweka vituo katika mikoa toafauti nchini, ili kuwahamasisha wanufaika namna ya kulipa madeni yao, kwa kuanzia mikoa ya Dar es salaam na Arusha.

Aidha Bodi ya mikopo imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha waajiri kutuma asilimia 15 ya mshahara wa wafanyakazi wao kila mwezi kwa wale ambao hawajakamilisha madeni yao kwa bodi ya Mikopo.