Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 13Article 562975

Habari Kuu of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hili Ndilo Eneo Hatari Dar

RC Amos Makalla akiwa Kunduchi RC Amos Makalla akiwa Kunduchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Amos Makalla amelitangaza eneo la Kunduchi lenye Volcano ya Tope kuwa eneo la hatari na halifai kwa makazi na kuwataka Wananchi wa familia Tisa ambazo makazi yao yameathiriwa kuanza kuchukuwa tahadhari.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo hilo kujionea athari za Volcano hiyo na kulielekeza Jeshi la Polisi kuweka uangalizi Katika eneo hilo.

Aidha RC Makalla amesema taarifa ya kitaalamu iliyowasilishwa ofisini kwake inaeleza kuwa eneo hilo halifai kwa makazi ndio maana amefika kuwataka kuchukuwa tahadhari wakati Serikali inaangalia hatua za kuchukuwa. Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza eneo hilo kuwekewa alama za tahadhari ili kuwaepusha wananchi na maafa.