Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540361

Habari za Mikoani of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Homera ataka takwimu wakulima waliofikiwa

Homera ataka takwimu wakulima waliofikiwa Homera ataka takwimu wakulima waliofikiwa

Homera ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho wa Kilimo biashara yaliondaliwa na  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI)  kwa kushirikiana na wadau wakiwamo Baraza la Nafaka Ukanda wa Afrika Mashariki.

 Amesema atakatembelea kila Halmashauri na Kata kukagua vitabu vya maofisa Ugani ambavyo vitaonesha idadi ya wakulima waliowafikia kuwapa elimu ya kilimo chenye tija.

"Kila Ofisa Ugani ajiadae kuonyesha idadi ya wakulima aliowafikia, kuna tatizo kubwa kwao  wanashinda ofisini mishahara wanapata vitendea kazi wanavyo sasa ama zangu au zao nitashuka nao jumla jumla wao chonjo, nahitaji wakulima wapate elimu ya kilimo bora ili kujikwamua na umasikini," amesema Homera

Afisa Kilimo Halmashauri Jiji la Mbeya, Erick Mvati amesema wako tayari kuteleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha maafisa ugani wanawatembelea wakulima.

Mwakilishi wa Baraza la Nafaka Ukanda wa Afrika Mashariki, Prudence Gerald amesema kuna mahitaji makubwa ya zao la Soya nchini ambapo kwa sasa uzalishaji ni tani 2,200  na hitaji kwa soko  ndani ni tani 150,000 hivyo aliwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji.

Join our Newsletter