Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560491

Habari Kuu of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Hotuba ya Rais Samia Yatajwa Katika Hotuba Bora za UN

Hotuba ya Rais Samia Yatajwa Katika Hotuba Bora za UN Hotuba ya Rais Samia Yatajwa Katika Hotuba Bora za UN

HOTUBA ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania aliyoitoa Septemba 23 kwenye Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) huko New York, imetajwa kuwa miongoni mwa hotuba saba muhimu zaidi kwenye kikao hicho.

Hotuba ya Rais Samia imechaguliwa na tovuti ya Marekani ‘Foreign Policy (FP)’ miongoni mwa hotuba muhimu zaidi kutolewa kwenye kikao hicho na pia ni ya pekee kutoka kwa mkuu wa nchi mwanamke.

Samia amekuwa mmoja wa wakuu wachache wa nchi wanawake kutoka Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Viongozi wengine ambao hotuba zao zimeelezea mambo muhimu ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Lebanon Michel Aoun, Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Katika chapisho lao ‘FP’ liliwataka wachangiaji na waandishi wa kurasa zao kupima hotuba wanazoona zina uzito mkubwa au zina mambo muhimu zaidi.