Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573703

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: millardayo.com

Hujachanja huingii baa

Hujachanja huingii baa Hujachanja huingii baa

Ripoti mpya kutoka nchini Kenya zinaeleza ya kuwa huenda sasa Baa pakawa pagumu kwa wasiochanja na wakaamua kunywea pombe zao majumbani kutokana na masharti mapya ya Covid 19 ambayo yamewafanya Wamiliki wa Baa na Hotel kulalamika kuwa itawapunguzia Wateja.

Serikali nchini Kenya imesema kuanzia December 21,2021 Watu watalazimika kuonesha cheti kuwa wamechanjwa chanjo ya Covid 19 ili kuruhusiwa kupata huduma kwenye Hotel, Baa, Migahawa, Maeneo ya Hifadhi na Mbugani na maeneo mengine ya biashara ambayo yanabeba zaidi ya Watu 50 kwa siku.

Shughuli zote zinazofanyika kwenye kumbi za ndani ikiwemo harusi na sherehe nyingine zenye kukusanya Watu zaidi ya 50 pia zitahusisha Watu kuonesha vyeti vya chanjo ya Covid 19, Wahudumu pia wa maeneo hayo yote ya Baa, Hotel n.k watapaswa kuwa na vyeti vya chanjo.