Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573310

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hujafa Hujaumbika, Kisa cha Huyu Kijana Utamwaga Machozi

Kijana Daniel Kijana Daniel

Huyu ni kijana Daniel (26) ambaye simulizi ya Maisha yake itakutoa machozi, jana Jumapili, Novemba 21, 2021, Daniel alifanya Kipindi na Dr. Isaac Maro wa Clouds FM, kupitia Kipindi cha Njia Panda ambapo ameeleza mengi kuhusu aliyopitia na kumfanya aonekana kama unavyomuona kwenye picha hii. Daniel alipata ajali ya kupigwa na shoti ya umeme, wakati akiwa kwenye fuso mkoani Kilimanjaro Moshi. Alikuwa yeye na wenzake juu ya fuso ambapo nyaya zenye moto zilimvuta na kusababisha cheche kubwa, gari liliungua na kuteketea palepale. Siku hiyo walikuwa watu watatu, dereva, yeye kama unavyomwona, na mwenzake ambaye katika tukio hilo alipona japo kwa sasa naye pia ni chizi kwa ajili ya tukio hilo la ajali. Kwa mjibu wa Dany, kwa sasa amepona kabisa, ila changamoto ni kipato kwani watu humwogopa kumpa kazi, na wengine kumwona kama mlemavu asiyeweza kazi, lakini ana uwezo wa kufanya Kazi, japo ana changamoto za upumuaji kwa njia ya pua, hutumia mdomo kufanya hivyo. "Natumia mdomo kwa kula na kupumua, wakati nakula, inanilazimu nile haraka kisha nipumue, hivyo hivyo mpaka namaliza kula,” amesema Daniel. Anaomba Watanzania wenye mapenzi mema wamsaidie kwani anapoishi hapana usalama na kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam. Kwa aliyeguswa, ajaribu kuwasaliana na Uongozi wa Clouds Media kwa urahisi Zaidi.