Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560437

Habari Kuu of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hukumu kesi ndogo ya ugaidi dhidi ya Mbowe kutolewa October 19

Hukumu kesi ndogo ya ugaidi dhidi ya Mbowe kutolewa October 19 Hukumu kesi ndogo ya ugaidi dhidi ya Mbowe kutolewa October 19

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake akiteta jambo na baadhi ya mawakili wake baada ya kesi kuahirishwa.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi inatarajia kutoa uamuzi Oktoba 19, 2021 wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi baada ya Upande wa Utetezi kufunga ushahidi katika kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.

Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi inasikilizwa na Jaji Mustafa Siyani ambaye atatoa uamuzi Oktoba 19, baada ya leo shahidi wa Utetezi, Lilian Furaha Kibona ambaye ni mke wa mshitakiwa Adam Kasekwa kumaliza kutoa ushahidi.

Uamuzi huo mdogo unatokana na pingamizi ambalo liliwekwa na Upande wa utetezi kuhusiana na kielelezo cha Upande wa Mashitaka kinachodaiwa kuwa ni maelezo ya mshitakiwa Kasekwa.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, washitakiwa wengine ni Halfan Bwire na Mohammed Ling’wenya.