Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554581

Siasa of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Hukumu ya Gwajima na Silaa Live Bungeni - Video

Hukumu ya Gwajima na Silaa Live Bungeni - Video play videoHukumu ya Gwajima na Silaa Live Bungeni - Video

SAKATA la wabunge Askofu Josephat Gwajima na Jerry Silaa limetua bungeni na leo Jumanne mchana mbivu na mbichi itajulikana kuhusu hukumu yao.

Mbunge wa Viti Maalum, Shally Raymond amewasilisha taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu wabunge hao.

Hii ni mara ya kwanza katika Bunge la 12 kamati kutoa taarifa yake mbele ya Bunge kwa wabunge waliohojiwa ingawa mbunge wa kwanza kuitwa mbele ya kamati hiyo alikuwa mbunge wa viti maalum, Felista Njau lakini taarifa yake haijawahi kusomwa hadharani.

Kanuni za Bunge zinatoa nafasi kwa Bunge kupokea taarifa kwanza kabla ya kuisoma na kuijadili kwa wabunge wote, hivyo baada kamati hiyo itawasilisha taarifa kamili na kujadiliwa bungeni.

Shally ameanza kuwasilisha taarifa ya Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima ambaye alisema anatuhumiwa kwa makosa ya kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge. Kwa upande wa Silaa amesema miongoni mwa tuhuma zake ni kuchonganisha wananchi na Bunge.

Wawili hao waliitwa mbele ya kamati mwanzoni mwa wiki iliyopita ambao kila mmoja alihojiwa kwa siku mbili tofauti huku kukiwa na vioja vya kukataa viti walivyopangiwa na wakati mwingine kuhojiwa wakiwa wamesimama.

Hukumu ya kamati hiyo huwa ni mapendekezo ya mbunge kusimamishwa vikao kadhaa na kutolipwa posho.

Katika Bunge la 11, miongoni mwa waliopitiwa na adhabu hiyo walikuwa Godbles Lema, Halima Mdee, Zitto Kabwe na Ester Bulaya.