Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584986

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Husna Mlanzi wa ITV Afariki Kwenye Ajali ya Simiyu

Husna Mlanzi Husna Mlanzi

Waandishi wa ITV Husna Mlanzi na Antony Chuwa ni kati ya waandishi wa Habari watano waliofariki Dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea leo Januari 11 mkoani Simiyu.

Waandishi wengine waliothibitika kufariki katika ajali hiyo ni Mwandishi wa kituo cha Uhuru Digital Johari Shani, Vanny Charles mtangazaji wa kituo cha mtandao Cha Icon Tv, na Afisa Habari wa Mkoa wa Mwanza Abel Ngapemba, Na Afisa Habari Ukerewe Steven.

Taarifa zilizotufikia hadi sasa ni kuwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo imefikia watu 14 huku waandishi wa sita wakipoteza maisha