Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544738

Habari Kuu of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

IGP Sirro Afanya Mabadiliko ya Makamanda

IGP Sirro Afanya Mabadiliko ya Makamanda IGP Sirro Afanya Mabadiliko ya Makamanda

MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa kuwahamisha na kuwapangia kazi makamanda wa polisi watatu kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye mikakati ya kubaini, kuzuia na kukabiliana na uhalifu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime, waliohamishwa ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Konyo ambaye ametolewa Kitengo cha Maadili Makao Makuu ya Polisi Dodoma na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Maigwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, amehamishiwa Mkoa wa Kilimanjaro huku Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Amon Kakwale aliyekuwa RPC wa Kilimanjaro, akihamishiwa Kamisheni ya Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi Dodoma.