Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552055

Habari Kuu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

IGP Sirro: Hatujapata Taarifa Rasmi Ili Kumkamata Gwajima

IGP Sirro: Hatujapa Taarifa Rasmi Ili Kumkamata Gwajima IGP Sirro: Hatujapa Taarifa Rasmi Ili Kumkamata Gwajima

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi linaendeshwa kwa maandishi hivyo wanasubiri barua kutoka kwa Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.

Maelekezo ya Waziri kutaka Jeshi la Polisi kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima yameonekana mtandaoni hivyo wanasubiri agizo rasmi.

IGP Sirro amesema katika kutekeleza agizo wataangalia kama kuna jinai kabla ya kufungua Mashtaka Mahakamani.

“Hatujapa taarifa rasmi ya maandishi ya kutakiwa kumkamata Mhe. Gwajima, lakini hata tukiipokea tutachunguza iwapo matamshi yake yanaangukia kwenye jinai, lakini tunaweza kuwashauri wakatatua jambo hili kwa njia za mazungumzo badala ya Polisi.

“Sisi kama polisi hatuna nafasi ya kufanya lolote kumhoji mtu pale anaposema maneno yasiyo na jinai ndani yake….” – majibu ya IGP Simon Sirro kufuatia agizo la Waziri wa Afya, Dk. Doroth Gwajima kulitaka Jeshi la Polisi na Takukuru kumhoji Askofu Josephat Gwajima kutokana na kauli zake za kupinga hadharani chanjo ya Uviko-19.