Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540154

Habari Kuu of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

IGP Sirro: Kinondoni Inaongoza kwa Uhalifu - Video

IGP Sirro: Kinondoni Inaongoza kwa Uhalifu - Video play videoIGP Sirro: Kinondoni Inaongoza kwa Uhalifu - Video

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni unaongoza kwa Uhalifu hapa Nchini. Ametaja baadhi ya vitendo kuwa wizi wa simu, uvunjaji na uporaji wa kutumia nguvu.

Amesema hayo akiwa Dar es Salaam wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata na Watendaji wa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.

Ameeleza, “Mtendaji wa Kata awajibike kwa nafasi yake kuhakikisha Amani na Usalama vinakuwepo katika Kata yake. Asipowajibika hana sababu ya kuwa Mtendaji wa Kata….”

Aidha, amesema kazi ya Mwenyekiti wa Mtaa sio tu kupiga mihuri, bali kazi ya kwanza ni Amani na Usalama.

Join our Newsletter