Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553225

Uhalifu & Adhabu of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

IGP Sirro, Sabaya kutoa ushahidi kesi ya Mbowe

Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA na Lengai Ole Sabaya aliekuwa Mkuu wa Wilaya Hai Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA na Lengai Ole Sabaya aliekuwa Mkuu wa Wilaya Hai

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro wanatarajia kuwa mashahidi kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Hatua hii inakuja mara baada ya Mbowe kusomewa mashtaka hii leo huku miongoni mwa hayo likiwemo shitaka la kutaka kumdhulu Sabaya, kipindi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Hata hivyo kesi hiyo imehamishiwa Mahakama Kuu mara baada ya idadi ya mshahidi kuwasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu mbeye ya Hakimu Mkuu Thomas Simba.