Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 04Article 561313

Habari Kuu of Monday, 4 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

IGP Sirro: Tutaimarisha usalama EAPCCO

IGP Sirro:  Tutaimarisha usalama EAPCCO IGP Sirro: Tutaimarisha usalama EAPCCO

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) litaendelea kuimarisha hali ya usalama kwenye nchi za shirikisho hilo kwa kufanya operesheni za pamoja na kuhakikisha wanadhibiti uhalifu unaovuka mipaka na kwa kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo alipokutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa DRC Congo, IGP Dieudonne Bahigwa ambaye amefanya ziara ya kikazi hapa nchini ikiwa ni siku chache kabla ya kupokea kijiti cha Uwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Masharika Mwa Afrika lenye jumla ya nchi 14 wananchama wa shirikisho hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DRC CONGO, IGP Diedonne Bahigwa, amesema, ziara yake imelenga kujifunza namna ambavyo IGP Sirro alivyofanikiwa kuliongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka miwili huku IGP huyo wa Congo akiahidi kuendeleza ushirikiano wa pamoja juu ya kuweza kufuatilia uhalifu unaofanyika kwenye ziwa Tanganyika na maeneo mengine.