Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544750

Habari Kuu of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

IMF kuisaidia Tanzania Fedha za Corona

IMF kuisaidia Tanzania Fedha za Corona IMF kuisaidia Tanzania Fedha za Corona

SHIRIKA la Fedha Duniani (IFM) limesema lipo tayari kuendelea kufanya kazi na wataalamu wa Tanzania kuandaa andiko litakalowezesha kupata msaada wa fedha kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na ugonjwa wa Corona.

Mkurugenzi wa Idara wa Afrika, Abebe Aemro Selassie, kutoka IMF ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Rais Samia Suluhu, Ikulu Chamwino, Dodoma.

Amesema IMF itasaidia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta zilizoathirika na ugonjwa wa |Corona ikiwa ni pamoja na sekta ya utalii, Maji na Afya na kwamba shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufikia maendeleo yanayokusudiwa.

Kwa upande wa Rais Samia, amesema kupitia Kamati Maalum aliyounda kukabiliana na ugonjwa wa Corona itashirikiana na Wizara ya Fedha kuandaa mpango wa jinsi ya kutekeleza maazimio ya ripoti maalum kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Rais Samia ameishukuru IMF kwa kuendelea kufanya kazi na serikali yake kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa kimaendeleo.