Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559972

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

IMF yatoa tahdhari kuporomoka kwa uchumi nchini

IMF yatoa tahdhari kuporomoka kwa uchumi nchini IMF yatoa tahdhari kuporomoka kwa uchumi nchini

Shirika la Fedha Duniani IMF, limetoa tahadhari ya kuanguka kwa uchumi wa Tanzania katika miezi 12 ijayo kufuatia madhara ya ugonjwa wa Corona yaliathiri mfumo mzima wa biashara nchini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Tanzania itahitaji msaada wa haraka wa kifedha wa dola bilioni 1.1 sawa na trilioni 2.39 za kitanzania ambazo ni asilimia 1.5 ya pato la Taifa.

Katika ripoti hiyo namba 21/213 ya mwezi Septemba 2021, imesema kuwa Tanzania inahitaji msaada wa haraka wa kifedha (BOP) wakati Serikali ikiwa inatekeleza mapango kamili wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao kwa ukubwa umeathiri usafirishaji wa bidhaa kimataifa.

"Uagizaji wa vifaa tiba vya dharura, vifaa vya maabara, na vifaa vya kujikingia unatakiwa kufanyika kwa haraka sana ili kuweza kupambana na wimbi hili la tatu la Corona, upatikanaji na usambazwaji wa chanjo unapaswa kupewa kipaumbele sambamba na kuboresha mazingra na miundombinu ya kutoa chanjo hiyo" imesema ripoti ya IMF.

Taarifa hii ya dharura imetolewa baada ya Bodi ya IMF mnano septemba 7, 2021 kuidhinisha kutolewa kwa dola milioni 567.25 sawa na shilingi bilioni 1.31 za kitanzania kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi uliosababisha na ugonjwa huo