Uko hapa: NyumbaniHabari2021 04 28Article 535684

Advertorial of Wednesday, 28 April 2021

Chanzo: eatv.tv

IPP yang'ara tuzo za Wanawake mahiri katika Habari

IPP yang'ara tuzo za Wanawake mahiri katika Habari IPP yang'ara tuzo za Wanawake mahiri katika Habari

Katika kutambua na kuthamini mchango wa Wanahabari Wanawake Nchini Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya habari utamaduni Sanaa na Michezo imetoa tuzo kwa Wanahabari Wanawake ambao wamegusa maisha ya watu wengi-

Submitted by Martha Magawa on Jumanne , 27th Apr , 2021 Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhaville akipokea tuzo, Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Lydia Igarabuza akiwa ameshikilia tuzo yake (katikati) na kushoto ni Beatrice Bandawe Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe.

kupitia kalamu zao ikiwemo Wanahabari wandamizi wa Makampuni ya IPP.

Wanahabari Wanawake waliopatiwa tuzo hizo ni ishirini na tano ambao ni pamoja na Mkurugenzi wa ITV Radio One Joyce Mhavile, Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Lydia Igarabuza na Beatrice Bandawe Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe.

Akizungumza wakati akiwakabidhi tuzo hizo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Dkt. Ally Possi amesema kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mwezi Mei, wanahabari wanatakiwa kufanya kazi kwa kutambua wajibu wao ni upi kabla ya kudai haki zao.

"Naomba nitoe wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanaendesha vyombo vyao kwa kuzingatia manufaa ya umma, kwa kutumia teknolojia za kisasa huku wakishirikisha wanawake kwani, wanawake wanaweza tena zaidi ya sana", amesema Dkt. Possi.

Kwa upande wao waliopata tuzo hizo wakatoa neno kwa Wanahabari chipukizi na masuala mazima ya uongozi ambapo wamesisitiza kufanya kazi kwa bidii na nidhamu kwa kila anayekuzunguka.

Join our Newsletter