Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559825

Habari za Afya of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Idadi ya wagonjwa wa akili itakua kubwa ndani ya miaka 10

Wagonjwa wa akili kuongezeka kwanzia miaka kumi ijayo Wagonjwa wa akili kuongezeka kwanzia miaka kumi ijayo

Kupitia tafiti zilizofanywa na wataalamu wa afya zinaonyesha kuwa ndani ya miaka kumi au ishirini ijayo kutakuwa na wagonjwa wengi wenye msongo wa mawazo pamoja kuongezeka kwa wasiwasi kwa sababu ya kuwepo kwa janga hili la UVIKO 19

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa maswala ya Afya kutoka wizara ya afya Dkt Irene Kindole ambapo amewasisitiza Wananchi kujitokeza kupata chanjo ya Corona ili kuondoa ugonjwa huo ambao unajulikana kama ugonjwa wa akili.

Aidha Mratibu wa matibabu wa magonjwa ya mlipuko pamoja na ugonjwa wa Corona Dkt Alex Sande amewasihi wananchi watumie fursa hiyo ya kuchanjwa ili kuendelea kuishi kwa amani kuliko kupatwa na ugonjwa wa msongo wa mawazo