Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 10Article 542092

Habari Kuu of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

JKT yawaita makambini wahitimu wengine kidato cha sita

JKT yawaita makambini wahitimu wengine kidato cha sita JKT yawaita makambini wahitimu wengine kidato cha sita

Aidha Jeshi hilo limeongeza majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2021 kwenda kuungana na Vijana wenzao walioitwa hapo awali kuhudhuria mafunzo na kufanya idadi ya vijana walioitwa kwa mujibu wa sheria mwaka huu kufikia 40,000.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini hapa kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo,Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena amesema walitarajia kuwaita vijana 35,000 lakini waliotwa mpaka sasa jumla yao ni 40,000 huku akisistiza kuwa mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu.

"Naomba kusisitiza hapa,mafunzo ya vijana hawa kwa mwaka huu ni miezi mitatu tu na siyo mwaka mmoja kama ambavyo inasemekana hivi sasa,huko mitaani kuna watu wanasema mafunzo ni mwaka mmoja,hii siyo kweli" amesema Kanali Mabena.

Join our Newsletter