Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 09Article 584344

Habari Kuu of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

JWTZ Yakanusha Kuingilia Sakata la Spika Ndugai Kujiuzulu

Luteni Kanali Ilonda Luteni Kanali Ilonda

JESHI la Wanacnhi Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa inayosambazwa mitandaoni kuwa linaingilia kati sakata la aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kujiuzulu.

Kauli hiyo imetolewa na Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ

"Siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za kupotosha ambazo zimekusudia kuwahadaa Watanzania kupitia mitandao ya Kijamii hususan YouTube, kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anaingilia kati sakata la Mhe. Rais na Spika. Jambo ambalo siyo la kweli"

"Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika na linawaomba Wananchu kuzipuuza taarifa zilizowekwa kwenye mtandao huo kupitia kwenye channel inayojiita NEWS 24 zenye kichwa cha habari ‘‘KIMENUKA MKUU WA MAJESHI MABEYO ATOA AMRI NZITO KUJIUZULU KWA NDUGAI’’ na ‘‘MKUU WA MAJESHI MABEYO AINGILIA KATI SAKATA LA RAIS NA SPIKA’’

"Ukweli ni kwamba, kikundi cha Watu wachochezi kimetoa taarifa za uongo na uzushi kwa kutumia sauti isiyo ya Mkuu wa Majeshi huku wakiwaaminisha Umma kuwa ni sauti ya Jenerali Mabeyo kwamba aingilia kati sakata la Mhe. Spika"

"JWTZ linawaomba Umma wa Watanzania kutoziamini taarifa hizo na wazipuuze kwa kuwa ni taarifa za uzushi na uchochezi zinazotungwa na kusambazwa na kikundi cha watu wasioitakia mema nchi yetu kwa maslahi yao binafsi, Mkuu wa Majeshi hajatoa taarifa yoyote kuhusiana na yaliyozushwa kwenye mitandao kwa kuwa JWTZ halijihusishi kwa njia yoyote ile na masuala ya kisiasa na kamwe halitafanya hivyo" amesema Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda.