Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541858

Habari za Mikoani of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Jamaa alazimishwa amle kuku mbichi Rombo kisa wizi

Jamaa alazimishwa amle kuku mbichi Rombo kisa wizi play videoJamaa alazimishwa amle kuku mbichi Rombo kisa wizi

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 Sesari Dorcas mkazi wa kata ya Allen chini wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kupigwa nakulazimishwa kumla kuku mbichi aliyekutwa naye kwa madai ya kuiba kuku huyo.

Mama wa kijana huyo amesema mtoto wake alipokamatwa na walinzi wa usiku maarufu kama sungusungu aliamriwa kumla kuku huyo na kusema mtoto wake ana matatizo ya akili na alishasingiziwa kwa kosa la ulawiti lakini aliachiwa na mahakama baada ya kuonekana hana hatia.

“tukio hilo lilimkuta alikamatwa na walinzi wa usiku wakamlazimisha alikuwa hajapikwa akamla na manyoya yake yote,ufahamu wake hauko vizuri naomba serikali inisaidie mtoto wangu aachiwe” Lusia -Mama wa kijana

Join our Newsletter