Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 23Article 543937

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 23 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Jambazi sugu auawa "alishawahi hukumiwa miaka 30"

Jambazi sugu auawa Jambazi sugu auawa "alishawahi hukumiwa miaka 30"

“Leo maeneo ya Tabata Liwiti kikosi maalum cha Polisi cha kufuatailia na kuzuia ujambazi, kilifanikiwa kufuatilia nyendo za wahalifu, na wahalifu wakabaini wanafuatilia walikuwa kwenye pikipiki, walipobaini wanafuatailiwa Polisi walianza kufyatua risasi lakini” Kamanda Muliro

“Polisi waliwakimbiza na wahalifu wakaanguka na pikipiki, wawili wakaanza kukimbia huku wakifyatua risasi na Polisi wakawajibika kujilinda wakaanza kufyatua risasi ambazo ziliwapata katika sehemu mbalimbali za miili yao wakapata majereha makubwa wakakimbizwa Hospitali baada ya muda walipoteza maisha wakafariki” Kamanda Muliro

“Mmoja wahalifu baada ya upekuzi alikutwa na silaha pisto, bunduki hiyo ilikutwa na risasi nne na eneo la tukio yaliokotwa maganda ya risasi, baada ya uchunguzi wa awali ilibainika kuwa baadhi ya wahalifu wale alikuwemo mhalifu sugu ambaye amekuwa akijihusisha na vitendo ya kijambazi muda mrefu” Kamanda Muliro

“Alivyochunguzwa anajulikana kwa jina la Said Gongwe, kumbukumbu zilionesha mhalifu huyu 1995 aliwahi kutuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha akafikishwa Mahakamani akafungwa miaka 30” Kamanda Muliro