Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 19Article 572818

Uhalifu & Adhabu of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Jela kwa kuvamia shule ya wasichana na kujichua

Jela kwa kuvamia shule ya wasichana na kujichua Jela kwa kuvamia shule ya wasichana na kujichua

Kijana mmoja (38), raia wa Zambia aliyewahi kufungwa gerezani amehukumiwa tena gerezani kwa kosa la kuvamia shule ya watoto wa kike na kujichua mbele yao.

Kijana huyo anayetambulika kwa jina la Simwanza amehukumiwa na mahakama ya Kasama Magistrates Court iliyopo katika wilaya ya Nakonde jimbo la Muchinga nchiniZbia.

Inaelezwa kijana huyo alitenda kisa hicho mnamo Novemba 8, 2021 katika shule ya wasichana ya Kasama pale alipovamia shule hiyo na kuwakuta wasichana waliokuwa katika maeneo ya shule hiyo kisha kufungua sehemu zake za siri mbele yao na kuanza kufanya kitendo hicho cha aibu.

Wanafunzi hao wa kike walilazimika kutimua mbio mpaka kwa uongozi wa shule hiyo na kuutaarifu ambapo viongozi shuleni hapo walikwenda eneo la tukio na kumkuta kijana huyo.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Joe Somboko baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo aliamua kumhukumu kifungo cha miaka miwili na adhabu ngumu kama adhabu ya kitendo hicho.

Katika utetezi wake kijana huyo aliomba apunguziwe adhabu kwakuwa ni siku chache tu alikuwa ametoka gerezani.

Hata hivyo utetezi huo haukuzaa matunda kwakuwa ulitupiliwa mbali na kutakiwa kutumikia kifungo hicho.