Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 28Article 554188

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Jela miaka 40 kwa kunajisi mtoto wa miaka 3

Jela miaka 40 kwa kunajisi mtoto wa miaka 3 Jela miaka 40 kwa kunajisi mtoto wa miaka 3

KIJANA mwenye umri wa miaka 30, Idrissa Mustafa Khamis amehukumiwa kwenda jela miaka 40 kwa makosa mawili ya kulawiti mtoto wa miaka mitatu, pamoja na kumtorosha akiwa chini ya uangalizi wa wazazi wake.

Hakimu wa Mahakama ya Mwera, Zanzibar, Said Hemed Khalfani alimtia hatiani kijana huyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na watu 10 pamoja na wa upande wa utetezi uliokuwa na watu watatu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Khalfani alisema ana muhukumu kijana huyo kwenda jela miaka 40 kwa makosa mawili, ambapo kosa la kwanza la kumuingilia kinyume na maumbile mtoto huyo wa kiume atatumikia jela miaka 30 na kosa la kutorosha miaka 10.

Alisema adhabu hizo zinakwenda sambamba, hivyo mshitakiwa atatumikia jela miaka 30 kwa makosa mawili.

Awali, upande wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambao uliwakilishwa na Shumbana Mbwana ulidai kuwa, tukio hilo lilifanyika Unguja Ukuu Desemba 4, mwaka jana na kuripotiwa katika Mahakama ya Mwera Machi Mosi, mwaka huu kwa kufunguliwa mashtaka hayo.

Alidai kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Machi 15, mwaka huu na jumla ya mashahidi 10 waliwasilisha utetezi wao.