Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 21Article 552862

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: HabarLeo

Jela miaka 50 kwa kunajisi mtoto wa miaka mitatu

Jela miaka 50 kwa kunajisi mtoto wa miaka mitatu Jela miaka 50 kwa kunajisi mtoto wa miaka mitatu

Mkazi wa kijiji cha Nungwi, mkoa wa Kaskazini Unguja, Ussi Haji Omar (34) amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili ya kunajisi na kutorosha mtoto chini ya umri wa miaka mitatu.

Hakimu Nyange Makame Ali wa Mahakama ya Mahonda mkoa wa Kaskazini, alimtia hatiani Ussi kwa makosa mawili ya kunajisi ambayo atatumikia miaka 30 na kutorosha mtoto wa kike akiwa chini ya uangalizi wa wazazi wake kutumikia miaka 20 jela, huku akitakiwa kulipa fidia Sh milioni mbili kwa aliyetendewa.

Mwendesha Mashtaka wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Ali Juma alidai kwamba, Aprili 28, mwaka huu mshtakiwa alimtorosha mtoto huyo (jina linahifadhiwa) na kumpeleka kichakani na kutekeleza uovu wake.

Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea alikubali kosa na hivyo kuirahisishia kazi ya mahakama kutoa adhabu.

Hakimu Nyange alisema matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia yamekuwa yakisababisha athari kubwa kwa wanawake na watoto.

''Natoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine katika kupambana na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ambayo yamesababisha athari kubwa kwa watoto na wanawake,'' alisema.