Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 30Article 540598

Habari Kuu of Sunday, 30 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Jenerali Mabeyo ahimiza diplomasia ya uchumi

Jenerali Mabeyo ahimiza diplomasia ya uchumi Jenerali Mabeyo ahimiza diplomasia ya uchumi

HALI ya uwakilishi kati ya Tanzania na Afrika Kusini inaridhisha kiulinzi na kiusalama huku ubalozi uliopo nchini humo ukiendelea kukuza ushirikiano na nchi hiyo na eneo la uwakilishi.

Hayo yalisemwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini, Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi alipomkaribisha Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo aliyetembelea ubalozi huo jana.

Mabeyo yupo nchini humo kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini, Jenerali Solly Shoke zilizofanyika kitaifa jana Mjini Pretoria, ikiwa ni utaratibu uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha ushirikiano no hususan katika Diplomasia ya Ulinzi na Amani katika eneo la jumuiya.

Akitoa taarifa ya eneo la uwakilishi Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho, Balozi Milanzi alisema wanaendelea kukuza ushirikiano na nchi za eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania inavyoelekeza kuendeleza diplomasia ya kisiasa na kutekeleza diplomasia ya uchumi.

Jenerali Mabeyo aliielezea ziara yake kwa ujumla nchini Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio na kwamba yapo mambo aliyojifunza. Alimwambia Balozi kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan amelenga kuendeleza maendeleo ndani na nje ya nchi.

Alisema ili malengo yafanikiwe, kunahitajika ushirikiano baina ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi nyingine zote kufanya utekelezaji wa diplomasia uendelee kuleta mafanikio siyo tu kwa Serikali bali pia kwa wananchi .

Join our Newsletter