Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553771

Habari za Mikoani of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Jiji lipo Shwari"- RC Makalla

Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM. Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM.

Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, amezungumza kwa Mara ya Kwanza tangu kutokea kwa tukio la muhalifu jana Agost 25, 2021, aliyekuwa akiwashambulia polisi na kusababisha mauaji ya watu wanne, na kusema kuwa wakazi wa jijini humo wasiwe na wasiwasi kwani hali ni shwari.

Amesema kuwa tukio hilo limedhibitiwa kwa weledi mkuu, na kuwataka wakazi wote wa jijini humo kuwa watulivu wasubiri taarifa zaidi, lakini pia waendelee na shughuli zao za kujenga taifa kwani usalama umeimarishwa.

"Niseme tu kwamba jiji lipo shwari, na wananchi waendelee na shughuli, uchunguzi unafanyika na taarifa za kina zitatolewa pale utakapo kamilika, kila kitu kimedhibitiwa vizuri"-Amos Makalla, RC

Hata hivyo amelipongeza Jeshi la Polisi kanda ya Dar es Salaam kwa kazi kubwa walioifanya jana ya kuweza kumdhibiti muhalifu.