Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540430

Habari Kuu ya

Chanzo: ippmedia.com

Jinsi Mabilioni yalivyochotwa Hazina

Jinsi Mabilioni yalivyochotwa Hazina play videoJinsi Mabilioni yalivyochotwa Hazina

Akizungumza katika Kikao Kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu,Manaibu  Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Mei 27, 2021, Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi CP Salum Rashid Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika kwamba tuhuma si za kweli wahusika watarejeshwa kazini.

Majaliwa alizitaja baadhi ya tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika  Machi 31, Mwaka huu  kupitia vocha 30 ya sh.milioni 251  yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi hiyo maalum ni kazi gani na nani aliifanya hiyo kazi.

Amesema  siku hiyo hiyo  ya Machi 31 pia zililipwa  sh. milioni 198.8 kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Majaliwa  amesema Aprili 8 mwaka huu watumushi  27 wa  wizara hiyo walilipwa sh. milioni 44.5 zikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki nne. Pia  Aprili 13 mwaka huu zililipwa sh. Milioni 155.2 kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Aidha, Aprili 30 mwaka huu zililipwa sh. milioni 43.9 kwa ajili ya kuandaa  mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyo hiyo zililipwa sh  miloni 14.4 kwa ajili ya siku ya wanawake. Fedha nyingine sh. Milioni 43 zililipwa siku hiyo na kufanya  jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa shilingi milioni 101.8.

Amesema kuwa, Mei 1 asubuhi mwaka huu zililipwa  sh. milioni 184.1 na mchana zililipwa sh  milioni 264 zikiwa ni malipo ya kazi maalum. "Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho"

Aliongeza kuwa Mei 3 mwaka huu zililipwa sh. milioni 146.5 kwa  watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa Mpango Kazi wa Manunuzi kazi ambayo  ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku.Tarehe hiyo hiyo zililipwa  sh. milioni 171.2 kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Majaliwa  amesema sh. milioni 155 zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi. " Yaani hii kazi ya ukaguzi inaandaliwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani,  na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha  kisha mnakwenda kuzichukuwa huko mlikozihamishia."

Majaliwa amewataka watendaji wa Wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na alitahadharisha kuwa watakaoendelea kuchenza na pesa za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Join our Newsletter