Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 23Article 543970

Habari za Mikoani of Wednesday, 23 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jokate aeleza kwa nini Temeke kwake ni nyumbani

Jokate aeleza kwa nini Temeke kwake ni nyumbani Jokate aeleza kwa nini Temeke kwake ni nyumbani

Muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo alieleza kwenye salam zake amefurahi kurudi nyumbani. Hata hivyo leo Jumatatu Juni 23, 2021 ametoa ufafanuzi zaidi kwa nini amesema kwake Temeke ni nyumbani. “Kwenye salaam zangu kwa viongozi wenzangu wa Wilaya na Manispaa ya Temeke niliwaambia kuwa nimefurahi kurudi tena nyumbani Temeke. “Awamu hii nimerudi kwa ajili ya utumishi zaidi kwa wana Temeke wezangu na kwangu Temeke ni nyumbani sababu; Moja nilishiriki Miss Kurasini na Miss Temeke na Equator Grill, na Chang’ombe TCC ulikuwa ni uwanja wa nyumbani. Jingine ni kwamba “Nimesoma Shule ya Mt. Antoni Mbagala; nan pia nimeshuhudia mechi nyingi za Yanga SC akimpiga Simba SC Tanzania pale Uwanja wa Taifa kwa Mkapa.