Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585838

Uhalifu & Adhabu of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

#KESIYAMBOWE: Airtel yakamilisha kutoa ushahidi

Airtel yakamilisha kutoa ushahidi Airtel yakamilisha kutoa ushahidi

Shahidi wa tisa kwa upande wa jamhuri, Gladys Fimbari amemaliza kutoa ushahidi wake kwenye kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashitaka ya ugaidi namba 16 ya 2021 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Shahidi huyo ambaye ni Afisa Meneja Kitengo Cha Sheria katika Kampuni ya Airtel Tanzania amekamilisha sehemu ya pili ya ushahidi wake baada ya kuhojiwa na mawakili wa upande wa jamhuri ukiongozwa na Wakili Robert Kidando huku Upande wa Utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala.