Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552202

Habari za Mikoani of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kabla haujanunua nyumba hakikisha mita haidaiwi" - TANESCO

TANESCO yatoa Tahadhari ya Vishoka TANESCO yatoa Tahadhari ya Vishoka

Shirika la Umeme Tanzania,TANESCO, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, limewatahadharisha Wakazi wa wilayani humo kuwa Macho na Watu Wanaojifanya Mafundi umeme Maarufu Vishoka ambao wamekuwa wakiingia katika nyumba na kuiba Mita za Umeme au kuchezea Mita hizo kwa nia ya Kujipatia Fedha kwa njia Isiyokuwa halali.

Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano Msaidizi wa Shirika hilo Mkoa wa Tanesco wa Kinondoni Kusini , Eddy Makobwe, kwa wananchi kutokana na Uwepo wa matukio ya Vishoka na kupata Malalamiko kutoka Kwa Wananchi.

Aidha amewataka wananchi wanaonunua vyumba au viwanja katika maeneo hayo kufatilia Tanesco kutokana na baadhi ya nyumba kubainika kuwa na madeni makubwa hivyo kuleta taharuki.