Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585445

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

"Kama humpendi Samia, penda nchi yako......" Samia

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Katikati ya vuguvugu linaloendelea hivi sasa nchini hasa kuhusu kundi linalodhaniwa kupinga utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia huku wengi wa wapingaji hao wakitajwa kuwa ni wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM hasa viongozi ambao wanashika nyadhifa mbalimbali za kiserikali.

Mapema hii leo Januari 13, 2022 wakati wa kikao cha Rais na Mawaziri pamoja na Manaibu jijini Dodoma, Samia amenukuliwa akisisitiza suala hilo katika muktadha tofauti.

Amesema kuwa Urais ni Taasisi ambayo inakuja na miongozo yake, na kuongeza kuwa kama miongozo hiyo inakidhana na matakwa binafsi ya mtu basi amchukie rais na sio nchi.

"Urais ni Taasisi yenye miongozo yake, kama humpendi aliyeko penda nchi yako"

"Muheshimu Mungu wako kwa kusimamia misingi ya nchi"....

"Samia aliyeko simpendi, mchukie yeye tu, ila penda nchi yako!" Amesema Kingozi huyo mkuu wa nchi"

Aidha amesisitiza pia juu ya uzito wa viapo ambavyo viongozi hao wameapa Januari 10, 2022 na kusema kuwa viapo hivyo ndio muhimili mkuu wa kazi na kuwa hakuna aliye mkamilifu.