Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 15Article 551572

Siasa of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kamati za Kudumu za Bunge kuanza vikao Jumatatu August 16, 2021

Kamati za Kudumu za Bunge kuanza vikao kesho Kamati za Kudumu za Bunge kuanza vikao kesho

KAMATI za Kudumu za Bunge zinatarajia kesho kuanza vikao vyake vya kawaida jijini Dodoma vitakavyohusisha uchambuzi wa taarifa, miswada mitatu ya sheria na Sheria Ndogo 163 kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge.

Katika vikao hivyo vitakavyofanyika jijini Dodoma na kukamilisha shughuli zake Agosti 29 kabla ya Mkutano wa Nne wa Bunge utakaoanza Agosti 31 mwaka huu, licha ya uchambuzi , kamati pia zitafuatilia masuala ya mapato ya serikali.

Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, ilisema uchambuzi wa miswada mitatu ya sheria utafanywa na Kamati tatu ambazo ni Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kamati ya Hesabu za Serikali na Kamati ya Katiba na Sheria.

Sheria Ndogo 163 zitakazochambuliwa ni zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Tatu wa Bunge na Sheria nyingine ndogo mbili zilizowasilishwa awali.

Kamati hizo za bunge pia zitafanya uchambuzi wa taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma kwa lengo la kuwezesha Bunge kufuatilia ufanisi na tija kwa mitaji ya serikali kwenye mashirika mbalimbali na taasisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchambuzi mwingine utakaofanyika ni wa taarifa za utendaji za Wizara kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza jukumu la kusimamia na kuishauri serikali.