Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553279

Habari Kuu of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Kamishna Mstaafu Kova aeleza tukio la Gwajima kubadilishiwa "Kiti na Microphone"

Kamishna Mstaafu Kova aeleza tukio la Gwajima kubadilishiwa play videoKamishna Mstaafu Kova aeleza tukio la Gwajima kubadilishiwa "Kiti na Microphone"

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova leo Agosti 23, 2021 kwenye Amplifaya ya Clouds FM ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokua vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.

“Wakati mwingine Mtu akishafanya jambo flani anakuwa na hisia flani ambazo sio za kawaida labda anafikiri nikikaa hapa naweza nikadhurika, ni tatizo la kisaikolojia kwa Mtu ambae ana msongo wa mawazo anakuwa hajiamini na haamini Mtu yeyote yule, kwahiyo anaweza kufanya jambo lolote lile”- Kamishna Mstaafu Suleiman Kova

“Mfano mimi zamani nilikua nahoji Wahalifu, akiletwa kwangu akisikia ni Kova anapoingizwa mule ndani anadondoka chini paap bila kumgusa, yani anaona amekutana na kitu cha hatari sana kutokana na yeye anavyoelewa, kama ni madhambi anayakumbuka yote” – Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.