Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540274

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kampuni za urasimishaji ardhi zatafuna bil 45/- za wananchi

Kampuni za urasimishaji ardhi zatafuna bil 45/- za wananchi Kampuni za urasimishaji ardhi zatafuna bil 45/- za wananchi

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema baadhi ya kampuni binafsi zinazofanya kazi ya urasimishaji ardhi zimechukua Sh bilioni 45 za wananchi bila kufanya kazi hiyo na kuzitaka zirejeshe fedha hizo.

Lukuvi alisema hayo bungeni Ddoma jana wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022.

Alisema kuna baadhi ya kampuni zinafanya kazi nzuri, lakini nyingine zinachukua fedha za wananchi bila kutekeleza kazi hizo.

“Tuliamua kushirikisha kampuni binafsi kurasimisha ardhi baada ya kuona tukifanya serikali peke yetu tusingefanikiwa, lakini kuna kampuni ziliweka bei za ajabu na tukafanikiwa kudhibiti.”

“Lakini kwa sasa kuna kampuni zimechukua fedha kwa wananchi zinafikia Sh bilioni 45 na hazijapima viwanja, ndio hao tunaopambana nao nataka niwahakikishie fedha hizo watazirudisha. Mimi sina nia ya kuwafukuza lakini lazima wananchi wapate haki zao,” alisema Lukuvi.

Kuhusu hoja ya wabunge ya wananchi kubomolewa nyumba baada ya kumaliza ujenzi badala ya kuzuia mapema, Waziri huyo alisema wizara hiyo inaangalia namna ya kuwatumia watendaji wa mitaa ili kuwabaini wanaovunja kanuni za mipango miji na kutoa taarifa mapema.

Alisema wizara hiyo imeandaa Sheria ya Nyumba na wanasubiri ipitishwe kwenye Baraza la Mawaziri na kuwa Sera ya Nyumba na kwamba yote yatakamilika mwaka wa fedha 2021/22.

Wakati bunge lilipokaa kamati, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alitaka kujua mkakati wa serikali wa kuwatetea wapangaji wanaopandishiwa pango na kuondolewa.

“Nilileta hoja na Bunge mwaka 2012 liliridha serikali ilete sheria ya kuwalinda wapangaji wa nyumba nchini dhidi ya dhuruma na uonevu wa kupandishiwa kodi, kulazimishwa kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka mzima na uwezekano wa kuondolewa wakati wowote,” alisema January.

Join our Newsletter