Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 27Article 566227

Habari Kuu of Wednesday, 27 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Karia amuangukia Rais Samia, vipimo MRI, Corona

Karia amuangukia Rais Samia, vipimo MRI, Corona Karia amuangukia Rais Samia, vipimo MRI, Corona

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemuangukia Rais Samia Suluhu kuingilia gharama za vipimo ambavyo timu za Taifa zimekuwa zikifanya mara kwa mara.

Rais wa TFF, Wallace Karia ametoa kilio chake hicho wakati wakikabidhi Kombe la Cosafa kwa Rais Karia leo, Oktoba 27,2021 mjini Dodoma

Akitoa ombi lake Karia amesema “Tumekuwa tukihitaji vipimo vingi vya MRI vya mara kwa mara kwa timu zetu za vijana, na pia vipimo vya Covid kama ambavyo unafahamu tunaishi kwenye ulimwengu wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona hivi sasa

“Gharama ni kubwa ukiangalia fedha tunazotumia tungeweza kufanya jambo lingine la maendeleo, MRI ni kutambua umri halisi wa vijana wetu, na Covid wamekuwa wakipimwa mara kwa mara timu inaposafiri, tunaomba tusaidie hili muheshimiwa Rais,”amesema

Aidha Karia amesema anaandaa dokezo ambalo atawapatia wasaidizi wake pamoja na viongozi wa Wizara ya Michezo ili liweze kusaidia