Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572566

Siasa of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Katibu Mkuu CCM ataka mabalozi kutambua wahamiaji haramu

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM ) Daniel Chongolo, Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM )

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amezitaka kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa kutumia mabalozi wa mashina kutambua wahalifu na wahamiaji haramu wanaoingia na kutishia amani na usalama.

Chongolo amesema mabalozi wa mashina wanakuwa na taarifa za kutosha zenye uhakika kuhusu wahusika halali wa maeneo yao na wasio wahusika kuanzia ngazi ya mashina na mpaka wilaya.

Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM katika shina namba sita la Kata ya Kanyonza Wilaya ya Kasulu Vijijini mkoani Kigoma ambapo amefika kwa ziara ya siku mbili kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

Amesema kuwa mabalozi hao kupitia vikao vyao vya mashina wana msaada katika kusaidia kupata taarifa sahihi kupanga mipango ya maendeleo ya wilaya na mikoa.

Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Anthony Mwakisu kueleza kuhusu uwepo wa mamia ya wahamiaji haramu kutoka Burundi kuingia katika wilaya hiyo na kuanza kujihusisha na shughuli mbalimbali ikwemo Kulima mashamba ya watanzania ndani ya Wilaya hiyo.

"Idara ya Uhamiaji imekuwa ikikamata wahamiaji haramu wakiwa nchini bila kibali. Tatizo hili ni kubwa Sana kwani mamia ya wahamiaji haramu kutoka Burundi ndio wanaolima mashamba ya watanzania wengi ndani ya Wilaya ya Kasulu," amesema Chongolo.

Kanali Mwakisu amesema Wilaya ya Kasulu imekuwa na wakimbizi zaidi ya 11,678 wa tangu 1972 walio katika Vijiji vya Kigadye, Kitanga na Munzeze Katika Wilaya katika Wilaya ya Kasulu ambao walihamia mwakan 2010 Kwa ajili ya kupewa uraia Ila mpaka sasa hatima Yao haijajulikana..