Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559999

Habari za Afya of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kauli ya Rais Samia kuhusu huduma ya chanjo nyumba kwa nyumba

Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa Tahadhari kuhusu Kampeni ya utoaji wa chanjo wa nyumba kwa nyumba inayoendelea mkoani Ruvuma kuwa isitumiwe vibaya kwa kuwalazimisha watu kuchanja.

Ametoa tahadhari hii mara baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Ofisa wa Afya wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma akipita nyumba kwa nyumba kutoa chanjo hiyo.

"Juzi na jana nilivyoingia nchini nimekuta hii agenda ya watu kupita nyumba kwa nyumba na mikoba ya sindano kuchoma watu, tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome, asiyetaka usichome, lakini kubwa nalotaka kusema mtu hana mamlaka ya kukubali au kukataa kama anayo elimu" Rais Samia

Nae Ofisa huyo amenukuliwa akitoa maoni ya kuitaka Serikali kuanzisha huduma itakayo wawezesha watu kuwaita watoa huduma ya afya kwa njia ya simu(mobile clinic) pindi wanapohitaji kupatiwa chanjo ya Corona.

Inaelezwa kuwa tayari Ofisa huyo amewaptaia watu 160 chanjo ya ugonjwa huo kwa siku moja pekee