Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553438

Diasporian News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kero 11 za Muungano zafutwa rasmi, bado 7

seleman Jafo, Waziri wa Muungano seleman Jafo, Waziri wa Muungano

Hoja 11 kati ya 18 za muungano zimepatiwa ufumbuzi na zitasainiwa hati za makubaliano ya kuziondoa kuwa miongoni mwa kero za muungano.

Utiaji wa saini hizo utashuhudiwa na makamu wa Rais, Dk Philip Mpango mjini Unguja, Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais muungano mazingira, Seleman Jafo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya vikao vya pamoja vya Serikali ya muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).