Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 551896

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kesi ya Kupinga Tozo za Miamala Yapigwa Kalenda

Kesi ya kupinga Tozo za Miamala Kesi ya kupinga Tozo za Miamala

Kesi ya kupinga tozo ya miamala ya simu iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) shauri la namba 11 la mwaka 2021 inayosikilizwa katikaMahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepigwa kalenda hadi tarehe 08 Septemba, 2021.

Mawakili upande wa Serikali wameweka pigamizi na kuiomba Mahakama kuifutilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa haina mashiko kwa kuwasilisha mapingamizi makuu matatu.

Mapingamizi hayo ni, Mahakama kuu haina uwezo wa kutoa nafuu ya tozo zilizoombwa, Madai hayo yamekosa sababu za msingi, na yamekosa ruhusa ya Bodi ya Madai.

Mahakama imesikiliza mapingamizi hayo ambapo upande wa serikali uliwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Wakili Gabriel Malata na upande wa mlalamikaji uliwakilishwa na Wakili Mpale Mpoki.