Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559249

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kesi ya Mbowe dhidi ya DPP na IGP kuendelea leo

Kesi ya Mbowe dhidi ya DPP na IGP kuendelea leo Kesi ya Mbowe dhidi ya DPP na IGP kuendelea leo

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Leo Septemba 23, 2021 saa nane mchana, inatarajia kutoa uamuzi mdogo kuhusu mapingamizi ya Serikali katika Kesi ya Kikatiba namba 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Mbowe amefungua kesi hiyo, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na IGP. akipinga hatua ya kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi ambapo kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilitajwa Agost 9, 2021.

Hata hivyo kiongozi huyo bado anashutumiwa kwa makosa hayo ya ugaidi katika Mahakama ya division ya Uhujumu Uchumi, akiwa ana wakilishwa na jopo la Mawakili wanaoongozwa na Wakili Peter Kibatala.