Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 554068

Uhalifu & Adhabu of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Sabaya yaaiairishwa

Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imeahirishwa katika mahakama ya hakimu mkazi arusha kutokana na nyaraka zinazoiwezesha mahakama hiyo kuendesha shauri hilo kutokukamilika.

Kwenye kesi hiyo Sabaya na wenzake Sita wanakabiliwa na Mashtaka manne huku mawili yakimkabili Sabaya peke yake.

Hakimu Patricia Kisinda aliyesikiliza shauri hilo ameahirisha kesi hiyo hadi September 9/2021

Mashtaka manne kwenye kesi hiyo ni Kuongoza genge la uhalifu, Uhujumu uchumi, Rushwa, na kujipatia fedha kinyume cha sheria makosa ambayo wanadaiwa kuyatenda mwaka huu eneo la Morombo jijini Arusha.