Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 554032

Uhalifu & Adhabu of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kijana akutwa akimbaka mwanafunzi wa miaka 10

Mwanafunzi wadarasa la nne aliyebakwa Mwanafunzi wadarasa la nne aliyebakwa

MALICK Apolonary (20) amekutwa amkimbaka kinguvu mwanafunzi wa darasa la nne (10) katika shule ya msingi Chanika iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo, Siriel Mchembe, ameagiza hatua kali na za haraka zichukuliwe kwa muhusika kwa kuwa ushahidi upo na amekamatwa katika eneo la tukio.

"Tukio la kijana Malick aliyekutwa akimbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10, ni tukio la wazi, ushahidi upo na amekamatwa eneo la tukio. Jambo hili limeniumiza kama mama na kama Mkuu wa Wilaya, na hata Rais Samia Suluhu jambo hili litamuumiza pia" amesema Mkuu wa Wilaya huyo.